June 21, 2011

MWALIMU ADAIWA KULAWITI MTOTO

Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Nyumbu, Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, (jina linasitiriwa kwa sasa), anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Temeke kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa shule ya chekechea mwenye umri wa miaka minne (jina linahifadhiwa).

Mwalimu huyo, mkazi wa Mtaa wa Mandela (zamani Wailes), Wilaya ya Temeke, anadaiwa kufanya kitendo hicho juzi mchana.

Mama mzazi wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa), alidai tukio hilo lilitokea juzi mchana, nyumbani kwake. Mwalimu huyo alikuwa mpangaji wake.

Alidai kuwa alibaini kubakwa kwa mwanaye baada ya kumtafuta bila mafanikio kwa lengo la kumuandaa kwenda madrasa.

Mama huyo alidai kuwa baadaye mtoto huyo alijitokeza na kueleza kuwa alikuwa chumbani kwa Mwalimu huyo.

Mtoto huyo alidai akiwa chumbani kwake, Mwalimu huyo alimlaza kitandani na kumvua nguo zote na kumfanyia kitendo hicho kisha kumweleza kuwa asimwambie chochote mama yake.

" Baada ya kumfanyia vibaya alimfundisha asiseme chochote. Lakini ni kama alikuwa kamfundisha aniambie, alipofika tu aliniambia nilikuwa kwa Mwalimu. Amenilaza kitandani, akanivua nguo na yeye akavua halafu...,” alidai mama huyo huku akilia.

Alidai kuwa walimuita Mwalimu huyo mbele ya mumewe na kukiri kumfanyia mtoto kitendo hicho kama alivyowasimulia.

Mama huyo alidai kuwa Mwalimu huyo alidai alifanya kitendo hicho baada ya kupitiwa na shetani.

Walitoa ripoti kituo cha Polisi Chang’ombe na kisha kumpeleka mtoto wake hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Alidai kuwa Polisi walimkamata mtuhumiwa huyo akiwa anahamisha vitu vyake kwenye vyumba alivyokuwa amempangisha.

Baadhi ya majirani waliomshuhudia Mwalimu huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi, walilaani kitendo hicho cha kinyama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, alipoulizwa jana, alisema hadi kufikia jana mchana, taarifa kuhusu kukamatwa kwa mwalimu huyo kutokana na kitendo hicho zilikuwa hazijafika ofisini kwake.

"Hiyo taarifa sina. Natoka kwenye kikao ndio narudi sasa hivi," alisema Kamanda Misime.

Chanzo Nipashe.

No comments:

Post a Comment